skip to main |
skip to sidebar
Askari watatu wauawa katika mapigano Libya
Mapigano kati ya watu wenye silaha na jeshi pamoja na polisi ya
Libya yamesababisha kwa uchache askari watatu kuuawa na wengine
kujeruhiwa. Mapigano hayo yametokea baada ya watu wenye silaha mjini
Bengazi mashariki mwa Libya, kufanya maandamano. Hayo yamethibitishwa na
kikosi maalumu cha jeshi la nchi hiyo kinachofahamika kwa jina la
‘Swaiqah’ na kuongeza kuwa, mapigano hayo yamejiri mapema leo asubuhi
ambapo katika mapigano hayo, kulitumiwa pia maguruneti na aina nyingine
ya silaha nzito. Aidha habari zaidi zinasema kuwa, mapigano yalijiri
baada ya waandamanaji waliokuwa na silaha kufanya shambulizi dhidi ya
ngome ya kilojestiki ya kikosi hicho cha Saiqah na kwamba, hadi sasa
bado milio ya risasi na milipuko inaendelea kusikika karibu na kambi ya
kikosi hicho cha Saiqah na askari wa miamvuli hapo mjini Bengazi.
No comments:
Post a Comment