Mkuu wa Muungano wa Wanawake wa Kiislamu nchini Russia
amesisitiza juu ya kutumiwa vazi la Kiislamu Hijab ya Kiislamu katika
maeneo ya umma bila ya kukinzana sheria hiyo ya Kiislamu na ile ya
serikali ya Russia. Nailya Ziganshina amesema kuwa, utumiwaji wa vazi la
Hijab kwa wanawake wa Kiislamu hakukinzani na sheria za sekta ya elimu
nchini humo, yakiwemo mashule. Bi Nailya Ziganshina amesema kuwa, uvaaji
huo wa Hijab unakwenda sambamba na mila, desturi na utamaduni wa kidini
katika jamii ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa, utumiaji wa Hijab
haukinzani na mafunzo kwa watoto kwenye shule za nchi hiyo. Inafaa
kuashiria hapa kuwa, ni miaka mingi sasa kwa serikali ya Russia kupiga
marufuku uvaaji wa Hijab kwenye mikusanyiko ya umma na hasa mashuleni ,
suala ambalo limesababisha matatizo makubwa kwa wafuasi wa dini ya
Kiislamu nchini Russia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment