skip to main |
skip to sidebar
Matokeo ya uchaguzi Madagascar kutotambuliwa
Serikali ya Ufaransa imetangaza kwamba, haitotambua
matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Madagascar iwapo wagombea fulani
watashiriki Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, Philippe
Lalliot amewataja rais wa sasa Andry Rajoelina, Lalao Ravalomanana; mke
wa rais wa zamani aliyepinduliwa na rais wa zamani Didie Ratsiraka na
kusema kwamba, kushiriki kwao kwenye uchaguzi ujao kutaendelea
kuitumbukiza Madagascar kwenye mgogoro wa kisiasa ulioanza mwaka 2009
kufuatia mapinduzi yaliyomuondoa madarakani, Mark Ravalomanana. Msimamo
wa Ufaransa unakwenda sanjari na ule wa Umoja wa Afrika AU na Jumuiya ya
SADC ambazo zimetaka wanasiasa hao kuheshimu makubaliano ya Maputo
yanayowazuia kuwania urais. Hii ni katika hali ambayo Mahakama ya kilele
ya Madagascar imeamua kwamba watatu hao wanaweza kuwania urais kwani
hakuna sheria ya nchi yao inayowazuia kufanya hivyo. Uchaguzi wa rais
unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
No comments:
Post a Comment