Rais Mohammad Mursi wa Misri ametangaza kuwa nchi yake imekata
kabisa uhusiano wa kidiplomasia na serikali ya Syria na kwamba ubalozi
wa nchi hiyo mjini Cairo utafungwa mara moja. Rais Mursi amekuwa
miongoni mwa viongozi wa Kiarabu waliochukua misimamo ya kufurutu mipaka
dhidi ya serikali ya Syria. Kwenye hotuba yake hapo jana mjini Cairo,
Mursi alisema atamuita nyumbani balozi wa Misri kufuatia uamuzi huo.
Weledi wa mambo wanasema hatua ya Misri itazidi kuvuruga hali ya mambo
nchini Syria haswa kwa kuzingatia kwamba Misri ilikuwa katika kundi la
nchi 4 zilizopewa jukumu la kufuatilia kadhia ya Syria kwa njia za
kidiplomasia. Nchi zingine kwenye kundi hilo ni Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran, Uturuki na Saudi Arabia. Huku hayo yakijiri, habari zinasema jeshi
la Syria limezidi kusonga mbele katika mji wa Allepo na kwamba
linaendelea kupata mafanikio makubwa. Hii ni katika hali ambayo,
Marekani inapanga kuanza kutuma silaha kwa magaidi wa Syria ili
kukabiliana na jeshi la nchi hiyo. Wakati huo huo, serikali ya Russia
imeionya Marekani dhidi ya kuweka marufuku ya kupaa ndege huko Syria
ikisema jambo hilo litakuwa ukiukaji wa sheria za kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment