Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, June 16, 2013

Watu wanne wauawa katika mlipuko Arusha, TZ


Eneo la mlipuko Arusha Juni 15 2013Kwa uchache watu watatu wanahofiwa kuuawa katika mlipuko wa bomu uliotokea mjini Arusha nchini Tanzania Jumamosi jioni katika mkutano wa kampeni wa chama kikuu cha upinzani Chadema.
Hujuma hiyo ya kigaidi ilijiri karibu saa 12 jioni kabla ya mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia wafuasi wa chama hicho katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha. Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania Advera Senso amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo.

Imearifiwa kuwa bomu hilo lililipuka karibu na jukwaa walikokuwa wamekaa wakuu wa Chadema. Mbunge wa chama Tawala CCM Hamisi Kigwangalla amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akitoa salamu zake za rambi rambia huku akisema amesikitishwa na mlipuko huo wa Arusha. Nawe Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe katika ukurasa wake wa Twitter amelaani waliohusika na hujuma hiyo na kusema serikali itatoa taarifa rasmi.
Hilo ni tukio la pili la bomu kulipuka hadharani mjini Arusha. Mnamo Mei 5 mwaka huu bomu lililipuka katika Kanisa Katoliki mjini humo na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment