Mufti wa Tunisia Sheikh Othman Battikh amesema wito wa Jihad
dhidi ya serikali ya Syria si sahihi kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na
ni kosa kubwa.
Akizungumza na waandishi habari siku ya Ijumaa, mwanazuoni huyo wa ngazi za juu Tunisia amesisitiza kuwa, 'Mwislamu hapaswi kupigana dhidi ya Mwislamu mwenzake' kwa kisingizio chochote kile.
Sheikh Battikh ametoa matamshi hayo baada ya kubainika kuwa vijana wengi wa Tunisia wanajiunga na mitandao ya kigaidi inayowatuma Syria kupigana dhidi ya serikali halali ya Rais Bashar al-Assad. Mwanazuoni huyo wa Tunisia aidha amesema kile ambacho sasa kinajulikana kama 'jihad ya ngono' ni zinaa na ukahaba. Amesema wasichana wadogo wa Tunisia wenye umri wa miaka 16 wamehadaiwa na kuenda Syria kushiriki katika kile Mawahabi wanakitaja kuwa ni ngono au ndoa ya jihad.
Amesisitiza kuwa kitendo hicho ni utovu wa maadili bora. Syria ilitumbukia katika machafuko Machi 2011 na idadi kubwa ya watu wameuawa na magaidi wanaopata himaya ya nchi za kigeni. Syria inazituhumu nchi za Magharibi na vibaraka wao katika eneo hasa Qatar, Saudi Arabia na Uturuki kuwa ndio waungaji mkono wakuu wa magaidi hao.

No comments:
Post a Comment