Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, April 4, 2013

Wasaudi milioni 10 hawana makaazi ya kudumu

Familia kubwa  Saudia inayoishi kwa umasikini katika makao duni
Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa karibu raia milioni 10 wa Saudi Arabia ambao ni asilimia 60 ya raia wote nchini humo hawamiliki nyumba.
Gazeti la Al Watan la Saudi Arabia limesema nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta inakabiliwa na tatizo sugu la kuwajengea wananchi hasa vijana nyumba bora za kuishi.
Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa asilimia 20 ya Wasaudi wanamiliki nyumba lakini katika mitaa duni. Katika miaka ya hivi karibuni Saudi Arabia imekumbwa na uhaba mkubwa wa nyumba kutokana na waliochukua mikopo kuchelewa kuilipa pamoja na ongezeko kubwa la bei ya ardhi pamoja na sheria ngumu za benki.
Mwezi Januari mwaka huu gazeti la Guardian la Uingereza lilisema kuwa idadi kubwa ya watu milioni 26 wanaoishi Saudi Arabia wanaishi katika umasikini. Huku umaskini ukiongezeka, kiasi kikubwa cha fedha za Saudia huishia katika mifuko ya ukoo wa Aal Saudi unaotawala nchi hiyo ya Kiarabu. Kwa mujibu wa Jarida la Forbes, utajiri wa mfalme wa Abdallah wa Saudia unakadiriwa kuwa dola bilioni 18 na hivyo kumfanya kuwa mfalme wa tatu tajiri zaidi duniani. Saudi Arabia pia ndie muuzaji mkubwa wa mafuta ya petroli duniani.

No comments:

Post a Comment