Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 8, 2012

Iran yalaani hujuma ya Wazayuni dhidi ya Al Aqsa

Iran yalaani hujuma ya Wazayuni dhidi ya Al Aqsa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Romin Mehmanparast amelaani vikali hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuhujumu na kuuvunjia heshima Msikiti wa Al Aqsa.
Mehmanparast amezitaka taasisi za kimataifa na kieneo hasa Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC kuchukua hatua kali dhidi uchokozi huo wa Wazayuni. Ametaka Wazayuni wazuiwe kuuyahudisha mji wa Quds na kubomoa Msikiti wa Al Aqsa ambao  ni kibla cha kwanza cha Waislamu.
Wakati huo huo Mahmoud Abbas rais wa Mamlaka ya Ndani ya  Palestina  ameitaka OIC iitishe kikao cha dharura kwa shabaha ya kujadili uvamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel na njama zake dhidi ya msikiti Mtakatifu wa al-Aqwa. Siku ya Ijumaa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel walitumia gesi za sumu na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waumini baada ya Sala ya Ijumaa katika msikiti  wa al-Aqsa mjini Quds.

No comments:

Post a Comment