Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 29, 2012

Daktari anayewatibu waliobakwa Kongo alengwa


Daktari anayewatibu waliobakwa Kongo alengwa
Polisi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamempeleka mahala salama daktari anayewatibu wanawake waliobakwa mashariki mwa nchi hiyo baada watu wenye silaha kufanya jaribio la kumuua.
Duru sinasema Daktari Denis Mukwege aliondolewa haraka kutoka mji wa Bukavu siku ya Jumamosi ambako amekuwa akiwatibu maelfu ya wanawake na watoto waliobakwa. Alkhamisi usiku watu watano wenye silaha
walimshambulia Muwkege akiwa nyumbani kwake hapo Bukavu na kumuua mlinzi wake. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali jaribio la kumuua Dk Mukwege ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Panzi katika mji wa Bukavu ulioko mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa DRC.
Ban ametoa wito kwa serikali ya DRC kuhakikisha usalama wa Dkt. Mukwege na familia yake, na kufanya kila iwezalo kuwakamata na kuwafikisha mahakamani walio jaribu kumuua daktari huyo.

No comments:

Post a Comment