HALI YA
TAHARUKI ILITANDA KATIKA MAENEO YA MKOA WA MJINI MAGHARIBI BAADA
YAKUENEA KWA TAARIFA ZAKUKAMATWA NA KUTEKWA NYARA NA WATU WASIOJUILIKANA
MSEMAJI WA JUMUIYA NA TAASISI ZAKIISLAM ZANZIBAR AMIRI FARID HADI
AHMED.
WAFANYABIASHARA WA MAENEO YA DARAJANI MJINI ZANZIBAR WALIKUFUNGA
MADUKA YAO WAKIHOFIA VITENDO VYA VURUGU VILIVYOANZA KUTOKEA KUFUATIA
KUKAMATWA KWA KIONGOZI HUYO.
BARABARAZA ZOTE ZA MAENEO YA MJINI ZILIWEKWA
MAWE NA KUCHOMWA MIPIRA YA GARI ILITOA MOSHI MWEUSI ULIOENEA KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MJINI NA HADI KUFIKIA AMANI KATIKA MAKUTANO YA BARABARA INAYOTOKEA UWANJA WA NGEGE KUELEKEA MTONI NA MWERA.
MAWE NA KUCHOMWA MIPIRA YA GARI ILITOA MOSHI MWEUSI ULIOENEA KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MJINI NA HADI KUFIKIA AMANI KATIKA MAKUTANO YA BARABARA INAYOTOKEA UWANJA WA NGEGE KUELEKEA MTONI NA MWERA.
VIJANA WA MAKUNDI MAOVU YA UBAYA UBAYA NA MBWA MWITU WAKIWA NA
MAPANGA WALIFANIKIWA KUJIINGIZA KATIKA KUNDI LA WAFUASI WA UAMSHO
WALIKUWA WAKIDAI KUACHIWA KWA SHEIKH FARIDI WAMEVUNJA BAA KADHAA ZA
MAENEO YA MJINI NA WILAYA YA MAGHARIBI.
VIJANA HAO WALIOJINASIBISHA NA UAMSHO WALIKUWA WAKINYWA POMBE NJIANI
BAADA YAKUKIMBIA NA KRETI ZA BIA NA BAADAE KUZIVUNJA KATIKA MAENEO YA
BARABARA ZA DARAJANI NA MJI MKONGWE WA ZANZIBAR.
POLISI WAKUTULIZA GHASIA WALIFANIKIWA KUTULIZA VURUGU HIZO MAJIRA YA
JIONI BAADA YAKURUSHA GESI YA KUTOA MACHOZI NA KUWATAWANYA WAFUASI WA
HARAKATI YA UAMSHO WALIOKUWA WAKIDAI KUACHIWA KWA KIONGOZI WAO.
AKIZUNGUMZA NA RADIO NOOR FM AMIRI MKUU WA JUMUIYA NA TAASISI
ZAKIISLAM ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH MSELLEM BIN ALI AMETHIBITISHA
KUTEKWANYARA KWA KIONGOZI HUYO NA KUONGEZA KUWA WANASHIRIKIANA NA JESHI
LA POLISI ZANZIBAR KUMTAFUTA.
AIDHA SHEIKH MSELLEM AMETOA MUDA WA SAA 24 KUACHIWA KWA KIONGOZI HUYO
ALIYEKAMATWA NA WATU WASIOJUILIKANA KABLA YA HARAKATI YAKE HAIJACHUKUWA
CHUKUWA HATUA ZINAZOFAA.
WAKATI HUO HUO NAKO MJINI DAR-ES-SALAAM KUMERIPOTIWA KUTOKEA
MAANDAMANO NA VURUGU KADHAA ZA WAISLAM BAADA YA JESHI LA POLISI
KUMKAMATA AMIRI WAKUTETEA HAKI ZA WAISLAM TANZANIA SHEIKH PONDA ISSA
PONDA.
No comments:
Post a Comment