Gari la Polisi la pili ambalo liliwachukuwa Viongozi wa Jumuiya ya
UAMSHO ambao walishitakiwa kwa makosa ya kufanya fujo na uchochezi
likiwa linasindikizwa na magari ya Polisi kuja Mahakama ya Wilaya ya
Mwanakwerekwe.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika
eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya
UAMSHO walipelekwa kwenda kusomewa mashitaka yao
Mmoja kati ya Viongozi wa UAMSHO Shekh Azan Khalid Hamdan (43) akishuka
kwenye gari la Polisi kuelekea Mahakamani Mwanakwerekwe kwenda kusomewa
mashtaka yao.
Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Shekh Farid Hadi Ahmed akishuka kwenye
gari la Polisi kuelekea Mahakama ya Mwanakwerekwe kwenda kusomewa
mashtaka yao yanayomkabili ikiwemo kusababisha fujo na uchochezi
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakiwa wanaimarisha usalama katika
eneo la Mahakama ya Wilaya Mwanakwerekwe ambapo Viongozi wa Jumuiya ya
UAMSHO walipelekwa kushitakiwa
Baadhi ya Wananchi walioenda Mahakamani hapo kwenda kushuhudia kesi
inayowakabili Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO ambao walikosa dhamana na
kurudishwa Rumande.
No comments:
Post a Comment