Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 29, 2012

Jonathan: Serikali ya Nigeria itapambana vikali ugaidi


Jonathan: Serikali  ya Nigeria itapambana vikali ugaidi
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amesema kuwa, serikali yake itapambana vikali na mashambulio ya kigaidi na vitendo vya utumiaji mabavu ambavyo vinahatarisha usalama wa nchi hiyo. Rais wa Nigeria amesema hayo katika radiamali yake kwa mlipuko wa jana katika mji wa Kaduna wa kaskazini mwa nchi hiyo ambao ulililenga kanisa moja mjini humo na kuuawa kwa uchache watu wanane. Amesema, serikali itaendelea kupambana na vitendo
vya kigaidi ambavyo vinaonekana kuwa tishio kwa usalama wa nchi hiyo. Mashambulio hayo ya jana kama ilivyo kwa mashambulio mengine ya miezi kadhaa nchini humo yamehusishwa na kundi la Boko Haram. Kundi la Boko Haram lilianza kuzishambulia taasisi za kiserikali, kama vile magereza, vituo vya polisi na shule katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria tokea mwaka 2009, na hadi sasa limeshaua zaidi ya watu 1,500.

No comments:

Post a Comment