Balozi wa Tanzania nchini Malawi amesema ramani mpya ya nchi yake
hailengi kupanua utata ulioko wa mpaka na nchi jirani ya Malawi.
Patrick Tsere ameongeza kuwa ramani ya Tanzania haijabadilika katika
maeneo ya mipaka na amesisitiza kwamba mabadiliko ya ramani ni ya ndani
kufuatia kubuniwa wilaya mpya. Mwezi uliopita Malawi ilijiondoa kwenye
meza ya mazungumzo na Tanzania baada ya serikali ya Dar es Salaam
kutangaza kwamba nchi ina ramani mpya. Lilongwe ilidai kwamba ramani
hiyo
imeathiri mpaka wa Ziwa Nyasa unaozozaniwa na pande mbili hizo. Malawi tayari imeiburuza Tanzania mbele ya vyombo vya sheria vya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kufuatia mvutano huo.
Na: Salim Swaleh

No comments:
Post a Comment