Katibu Mkuu wa chama cha upinzani
cha CHADEMA nchini Tanzania, Dkt. Willibrod Slaa amemkosoa Rais Jakaya
Kikwete akidai kuwa hana ubavu wa kupambana na rushwa kwa kuwa chama
chake cha CCM kiliingia madarakani kwa rushwa katika uchaguzi mkuu wa
mwaka 2005. Dkt. Slaa amesema rushwa inazidi kukua siku hadi siku nchini
Tanzania bila ya ikulu kuchukua hatua yoyote. Katibu Mkuu wa CHADEMA
amesema Rais Kikwete anatania kuhusu tatizo la rushwa kwa kulizungumza
tu majukwaani, huku akiwalinda washirika wake.
Dkt. Slaa amezungumzia
vitendo vya rushwa vilivyojitokeza katika uchaguzi wa viongozi wa CCM ni
kielelezo tosha kwamba, chama hicho hakina uwezo tena wa kupambana na
rushwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment