Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, October 23, 2012

Mwanamke mweusi achomwa moto Marekani



Mwanamke mweusi achomwa moto Marekani
Mwanamke wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika ameshambuliwa kwa kupigwa na kisha kuchomwa moto na kundi la vijana wenye fikra za kibaguzi katika jimbo la Louisiana nchini Marekani.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20 alishambuliwa na kuchomwa moto vibaya kifuani na miguuni na Wamarekani weupe akiwa anatembea ndani ya bustani ya Winnsboro huko Louisiana. Taarifa zinasema kuwa, watu
waliotekeleza shambulio hilo la kinyama walikuwa ndani ya gari lenye namba zilizoandikwa herufi tatu 'KKK' zenye maana ya Ku Klux Klan, ambalo ni kundi lililodhidi ya Wamarekani weusi.
Sharmeka Moffitt mhanga wa tukio hilo alitoa taarifa polisi na kusema kuwa, watu waliomshambulia walifunika nyuso zao kwa soksi maalumu. Mama wa Sharmeka ameeleza kuwa, mtoto wake yuko mahututi na amelazwa kwenye kituo cha LSU huko Shreveport. Luteni Julie Lewis Msemaji wa Polisi wa jimbo la Louisiana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusisitiza kwamba, asilimia 60 ya mwili wa mwanamke huyo imeharibika vibaya kwa moto kutokana na shambulio la kinyama lililofanywa dhidi ya mwanamke huyo mweusi.

No comments:

Post a Comment