Serikali ya Zimbabwe imeketi kwa shabaha ya kuchunguza rasimu ya
katiba mpya ya nchi hiyo. Taarifa zinasema kuwa, kupitiwa rasimu hiyo ya
katiba kunahesabiwa kuwa ni hatua muhimu yenye lengo la kumaliza
hitilafu kati ya Rais Robert Mugabe ambaye pia ni kiongozi wa ZANU PF na
Morgan Tsvangirai Waziri Mkuu ambaye pia ni kiongozi wa chama cha MDC.
Vyama hivyo viwili viliamua kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, baada
ya kuibuka machafuko yaliyosababishwa na matokeo ya uchaguzi wa rais wa
mwaka 2008. Taarifa zinasema kuwa uchaguzi ujao umepangwa kufanyika
mwezi Machi 2013, huku Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 88 akiwania
kutetea kiti cha urais. Hii katika hali ambayo, wataalamu wa kiuchumi
wanaeleza kuwa, hitilafu za kisiasa ni moja ya sababu kuu iliyopelekea
kuongezeka umasikini, ufukara na hali mbaya ya kimaisha na kiafya kwa
wananchi wa nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment