Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, ikiwa
mataifa ya eneo la Mashariki ya Kati na mengineyo yatathubutu kutenga
siku moja na kuitangaza kuwa ni siku ya kujibari na Marekani, basi bila
ya shaka yoyote mataifa hayo yatakuwa yamepiga hatua kubwa ya
kihistoria. Kiongozi Muadhamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameyasema
hayo Jumatano hii mjini Tehran alipokutana na maelfu ya wanachuo na
wanafunzi tofauti katika kukaribia kwa tarehe 13 Aban sawa na tarehe 4
Novemba, ambayo hapa nchini Iran inahesabiwa kuwa ni siku ya taifa ya
wanafunzi na kupambana na ubeberu wa kimataifa. Kiongozi Muadhamu
amewataka viongozi na wakuu wa mihimili mitatu ya dola yaani serikali,
bunge na mahakama nchini Iran, kufanya kazi kwa bidii na kwamba katika
kipindi hiki wanatakiwa kuwa makini katika utendaji wa kazi zao na
wajiepushe na masuala madogomadogo yanayoenezwa na makelele ya vyombo
vya habari vya Wamagharibi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment