Waziri wa Usalama wa Taifa nchini Kenya ameyaonya makundi
yanayozusha fujo nchini humo kwamba yatakabiliwa na mkono mrefu wa
sheria. Katoo Ole Metito amesema makundi kama MRC na mengine ambayo
yametishia kuvuruga uchaguzi mkuu ujao yatakiona cha moto iwapo
yataendelea kutoa matamshi ya kijuba kama hayo. Kiongozi huyo ambaye
aliteuliwa kuwa Waziri majuma kadhaa yaliyopita ameahidi kutembea kila
kona ya nchi ili kuhakikisha kwamba amani na utulivu vinatawala kabla,
wakati na baada ya uchaguzi mkuu ujao. Hii ni katika hali ambayo, Waziri
wa Uvuvi wa Kenya Amason Kingi alinusurika kifo siku chache zilizopita
baada ya mkutano wake kuvamiwa na vijana wanaodaiwa kuwa wanachama wa
MRC. Msemaji wa MRC Rashid Mraja hata hivyo amekanusha madai hayo na
kusema hizo ni njama za kuzima kilio cha kundi lake cha kutafuta haki za
Wapwani ambao wamenyanyaswa kwa muda mrefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment