Bomu kubwa lililokuwa limetegwa kwenye gari limeripuka leo katika
mtaa wa Ashrafia huko katikati mwa Beirut mji mkuu wa Lebanon na kuua
watu wanane na kuwajeruhi wengine 78. Bado haijafahamika wazi iwapo
mripuko huo ulikuwa umekusudiwa kumlenga shakhsia yoyote wa kisiasa wa
huko Lebanon au la. Mripuko huo mkubwa wa bomu umetokea katika mtaa
ambao una ofisi ya chama cha Kikristo cha Mafalanja kinachompinga Rais
Bashar Assad wa Syria. Polisi ya Lebanon imethibitisha kuuawa watu
wanane na kujeruhiwa wengine 78 katika mripuko huo wa leo. Magari na
majengo kadhaa pia yameharibiwa vibaya katika mripuko huo wa bomu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment