Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, October 28, 2012

Mpalestina auawa shahidi katika hujuma ya Israel



Mpalestina auawa shahidi katika hujuma ya IsraelMpalestina ameuawa shahidi na mwingine kujeruhiwa katika hujuma ya angani ya utawala haramu wa Israel huko Gaza.
Duru zinasema kuwa,  alfajiri ya leo, Israel imetumia ndege ya kivita isiyo na rubani (drone) kuvurumisha makombora katika mji wa Rafah.
Utawala wa kibaguzi wa Israel umeshadidisha na kupanua mashambulizi yake dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.  Ehud Barak Waziri wa Vita wa Israel amesema kuwa, wataendelea kufanya mashambulizi huko Gaza. Wapalestina milioni 1.7 huko Gaza wanishi katika mzingiro wa Israel tokea mwaka 2007 ambapo wananyimwa haki za kimsingi kama vile madawa, chakula, elimu n.k.

No comments:

Post a Comment