Serikali ya Uganda imelitaka kundi la M23 la Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo lisianzishe tena mapigano ambayo yamewalazimisha maelfu ya
wakimbizi wa Kikongo kuvuka mpaka na kuingia nchini Uganda. Wito huo
umetolewa na Okello Oryem, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda ikiwa
ni siku moja tu baada ya Harakati ya Waasi ya M23 kutishia kwamba,
itaanzisha tena mashambulio dhidi ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo. Okello Oryem amesema, Kampala inalitaka kundi
hilo kuheshimu usitishaji mapigano. Kundi la M23 lilisitisha mapigano
Agosti mwaka huu baada ya kukutana na Rais Yoweri Museveni mjini Kampala
na kutakiwa kufanya mazungumzo na serikali ya Kinshasa. Hata hivyo
Runninga Lugerero, mmoja wa viongozi waandamizi wa M23 alitishia
mwishoni mwa juma akiwa huko Bunagana kwamba, kundi lao litaanzisha tena
vita kutokana na kuwa, Rais Joseph Kabila wa Kongo hayuko tayari
kufanya mazungumzo ya amani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment