Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, October 30, 2012

Ujumbe wa Bunge la Iran kuitembelea Myanmar



Ujumbe wa Bunge la Iran kuitembelea MyanmarMsemaji wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Bunge la Iran amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na ujumbe wa Bunge la Iran utafanya safari nchini Myanmar katika siku zijazo. Seyyid Hussein Taqavihuseini sambamba na kuashiria jinai za kutisha na mauaji ya umati yanayofanywa dhidi ya Waislamu wa Myanmar amesema, kuendelea mauaji hayo ni jambo la kusikitisha lakini cha kusikitisha zaidi ni kukaa kimya taasisi za kimataifa na jumuiya za kutetea haki za biandamu ambazo hazijaonyesha radiamali yoyote kuhusiana na jinai hizo.
Taqavihussein amesema, kamati imeundwa na kamisheni hiyo kwa ajili ya kufuatilia hali ya Waislamu wa Myanmar na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Mambo ya Nje, Ali Akbar Salehi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anapanga kuitembelea Myanmar katika siku zijazo. Kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofaywa na Mabudha dhidi ya Waislamu wa Myanmar, watu wasiopungua 112 wameripotiwa kuuawa na huku maelfu ya wengine wakiyakimbia makazi yao.

No comments:

Post a Comment