Naibu Waziri Mkuu wa Kenya Bw. Musalia Mudavadi amesema kuwa,
Wakenya wanne wanaokabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya
Jinai (ICC), kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007
hawana hatia na kwamba makosa ni ya Wakenya wote. Bwana Mudavadi
amesisitiza kwamba, Wakenya wote walishiriki katika ghasia hizo za
uchaguzi. Amesema kama ninavyomnukuu, "Tuliuana wenyewe kwa wenyewe,
wanawake walibakwa na watoto kudhulumiwa, sote tunapaswa kuwajibika,
taifa zima lilihusika, hivyo kuwashtaki Wakenya wanne kwa niaba ya watu
milioni 40 sio haki.” Mwisho wa kumnukuu. Mudavadi amesema, washukiwa
hao, Uhuru Kenyatta, Mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto, Francis
Muthaura na mtangazaji Joshua Arap Sang wanapaswa kushtakiwa nchini
Kenya. Ameongeza kuwa, Wakenya wote wanapaswa kukubali makosa yao
yaliyopelekea kuzuka ghasia hizo. Aidha amesema, yeye alikuwa miongoni
mwa watu waliohimiza kubuniwa mahakama maalumu ya kuwashtaki washukiwa
wa ghasia za baada ya uchaguzi na kwamba, msimamo wake haujabadilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment