Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Luteni Kanali
Mussa Mrisho Mtengwa nyumbani kwa marehemu kijijini Kiwangwa,wilayani
Bagamoyo leo jioni wakati Rais Kikwete alipokwenda kushiriki mazishi ya
Marehemu.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu
Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa wakati wa mazishi yaliyofanyika
nyumbani kwa marehemu kijiji cha Kiwangwa wilaya ya Bagamoyo mkoani
Pwani leo jioni.
Enzi za Uhai wake Marehemu Luteni
Kanali Mtengwa aliwahi kuwa mpambe wa Rais wa awamu ya Pili Ali Hassan
Mwinyi,kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 1995.Marehemu aliwahi pia kufanya
kazi katika Wizara ya Sheria na kushika nafasi mbalimbali za uongozi
ndani ya jeshi.
Marehemu alifariki juzi tarehe 25
Oktoba nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam baada ya kuugua
kwa muda na ameacha mjane watoto wanne na wajukuu watatu(picha na Freddy
Maro).
No comments:
Post a Comment