Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 29, 2012

Iran yazitaka asasi za kimataifa zizuie jinai za Israel



Iran yazitaka asasi za kimataifa zizuie jinai za IsraelMsemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amezitaka asasi za haki za binadamu kuzuia  kuendelea jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya taifa madhulumu la Palestina. Ramin Mehmanparast amelaani mashambulio ya kigaidi ya hivi karibuni ya Israel huko Gaza na kusisitiza kwamba, jinai hizo zinazidi kubainisha utambulisho wa utawala huo ghasibu. Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amezitaka taasisi za
kimataifa hususan asasi za haki za binadamu kuchukua hatua za lazima ambazo zitazuia kuendelea jinai za Wazayuni dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.  Ramin Mehmanparast amezikosoa pia siasa za kindumakuwili za madola ya Magharibi kuhusiana na kadhia nzima ya Palestina na kulaani himaya na uungaji mkono wa madola hayo kwa utawala wa Kizayuni wa Israel unaotenda jinai kila uchao huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

No comments:

Post a Comment