Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, October 31, 2012

Mfumuko wa bei wapungua Kenya


Mfumuko wa bei wapungua Kenya
Mfumuko wa bei Kenya umepungua kwa kiasi cha chini zaidi katika kipindi cha miezi 23 iliyopita na hivyo kuibua matumaini miongoni mwa wananchi.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Kenya  (KNBS), pamoja na kuwepo ongezeko la bei ya mafuta ya petroli, mfumuko wa umeshuka hadi asilimia 4.14 mwezi Oktoba ikilinganishwa na asilimia 5.32 mwezi Septemba mwaka huu. Kiwango cha mfumuko wa bei Kenya sasa ni cha chini zaidi tokea Desemba mwaka 2010.
Katika taarifa  kaimu mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Kenya  Zachary Mwangi amesema kumeshuhudiwa kushuka bei ya vyakula kama vile sukuma wiki,mahindi, tomato na  karoti. Hatahivyo amesema kumeshuhudiwa ongezeko la bei ya baadhi ya bidhaa kama vile viazi, ndizi na nyama ya ng’ombe.
Weledi wa mambo wanasema mfumuko wa bei umepungua Kenya kutokana na ongezeko la uzalishaji wa vyakula, kupungua bei ya petrol kimataifa katika mizi iliyotnagulia na usimamizi bora ya kifedha.

No comments:

Post a Comment