Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
ameelezea wasiwasi wake kutokana na kuanza tena wimbi jipya la mauaji ya
Waislamu wa Myanmar na mapigano mengine ya kikabila nchini humo na
kuitaka serikali ya nchi hiyo kukomesha haraka iwezekanavyo machafuko
hayo. Ban Ki moon ametoa taarifa hiyo baada ya kuuawa kwa akali watu 56
katika jimbo la Rakhine na kuongeza kuwa, wimbi la machafuko lililotokea
hivi karibuni katika
miji mitano ya jimbo hilo ni lenye kuitia
wasiwasi mno jamii ya kimataifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
amesisitiza kuwa, serikali ya Myanmar inapaswa kuchukua hatua za haraka
zenye shabaha ya kukomesha machafuko nchini humo. Imeelezwa kuwa, mamia
ya nyumba zimeteketezwa kwa moto na wahalifu wa Kibudha kwenye jimbo la
Rakhine, huku maelfu ya watu wakiyakimbia makaazi yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment