Watu wasiopungua 15 wameuawa nchini
Iraq na makumi ya wengine kujeruhiwa katika wimbi jipya la mashambulio
ya kigaidi yaliyoikumba nchi hiyo. Maeneo yaliyokumbwa na mashambulio
hayo ya kigaidi ni al-Mushadah kaskazini mwa Baghdad na Fallujah katika
mkoa wa al-Anbar. Taarifa zaidi zinasema kuwa, mashambulio hayo ya
kigaidi yaliyotokea katika maeneo ya kaskazini na katikati mwa Iraq
yamezusha wasi wasi mkubwa baina ya wananchi. Mashambulio hayo yametokea
katika hali ambayo kwa majumaa kadhaa sasa Iraq imeshuhudia hali ya
utulivu wa kiwango fulani. Vyombo vya usalama vya Iraq vimeimarisha
usalama katika maeneo yaliyotokea mashambulio hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment