Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, October 11, 2012

Mashimo Al-Aqswa yatakuwa na matokeo mabaya


Mashimo Al-Aqswa yatakuwa na matokeo mabaya
Khatibu wa Masjidul Aqswa huko Palestina ametahadharisha kuhusiana na matokeo mabaya ya uchimbaji mashimo unaofanywa na Wazayuni kando kando ya msikiti huo mtakatifu. Sheikh Akram Sabri amesema kwamba, msikiti huo unakabiliwa na hatari ya kubomoka kutokana na mashimo na njia za chini kwa chini zinazochimbwa na Wazayuni chini na kando kando ya msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu.  Taarifa zaidi zinasema kuwa, licha ya makelele ya Walimwengu lakini kundi moja la Wazayuni bado linaendelea kuchimba mashimo chini ya msikiti huo na maeneo jirani.
Khatibu wa msikiti wa Al Aqswa amewataka Waislamu kuingilia kati na kuzuia siasa za kimabavu za utawala haramu wa Israel dhidi ya msikiti huo mtakatifu kibla cha kwanza cha Waislamu. Wakati hayo yakiendelea, wakazi wa mji huo hawaruhusiwi kujenga nyumba zao na badala yake utawala haramu wa Israel unaendelea na siasa zake za kubomoa na kuharibu maeneo ya kidini na kujenga sehemu ambazo zina nembo za Kiyahudi ikiwa ni njama za kufuta kabisa nembo za Kiislamu huko Baytul Muqaddas.

No comments:

Post a Comment