Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, October 25, 2012

Kura ya maoni ya katiba Zimbabwe kufanyika mwakani



Kura ya maoni ya katiba Zimbabwe kufanyika mwakani
Afisa wa ngazi za juu katika chama cha ZANU-PF nchini Zimbabwe amedokeza kwamba, kura ya maoni kuhusu katiba mpya huenda ikafanyika mwezi Januari mwaka ujao wala sio mwezi ujao kama alivyokuwa ameashiria Rais Robert Mugabe hivi majuzi. Paul Mangwana, mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia mchakato wa kupatikana katiba mpya amesema kuwa,
tofauti zilizoibuka mwanzoni mwa wiki kwenye mkutano wa kujadili rasimu ya katiba utasababisha kura ya maoni kucheleweshwa. Vyama 3 vinavyounda serikali ya umoja wa kitaifa vilishindwa kufikia makubaliano kwenye mkutano huo hususan kuhusu kipengee kinachogusia mamlaka ya rais na kile cha muundo wa jeshi. Mangwana amesema vipengee vyenye utata vinapaswa kujadiliwa kwa kina kabla ya kura ya maoni kufanyika.
Na: Salim Swaleh

No comments:

Post a Comment