Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, October 18, 2012

Sheikh Ponda atiwa mbaroni TZ kwa uchochezi

Sheikh Ponda atiwa mbaroni TZ kwa uchocheziDuru za habari nchini Tanzania zinasema kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Issa Ponda Issa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amenukuliwa akisema kuwa, Sheikh Ponda alikamatwa Jumanne usiku akikabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi dhidi ya Serikali iliyoko
madarakani.
Aidha imedaiwa kuwa amehusika na uchochezi wa udini kati ya Waislamu na Wakristo na ndani ya Waislamu wenyewe, kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani.
Jeshi la Polisi Tanzania limesema Sheikh Ponda atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Machafuko yameripotiwa maeneo kadhaa mjini Dar-es-Salaam kufuatia kukamatwa Sheikh Ponda.
Wakati huo huo vurugu zimetokea Zanzibar katika eneo la Michenzani na maeneo mengine ya karibu kufuatia kuenea ripoti kuwa msemaji wa taasisi za Kiislamu Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmad ametekwa nyara na watu wasiojulikana. Polisi Zanzibar wamekanusha madai kuwa wamemkamata Sheikh Farid.

No comments:

Post a Comment