Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 29, 2012

Wanajeshi 11 wa Somalia wauawa na Al-Shabab



Wanajeshi 11 wa Somalia wauawa na Al-Shabab
Kwa akali wanajeshi 11 wa serikali ya Somalia wameuawa katika mapigano baina yao na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab. Mapigano hayo yalizuka katika mji wa Afgoye wa kusini mashariki mwa nchi hiyo  na kwamba, kanali wa ngazi za juu wa jeshi ni miongoni mwa waliouawa katika mapigano hayo.
Mapigano hayo yanatokea siku chache tu baada ya vikosi vya kusimamia amani vya Umoja wa Afrika AMISON vikishirikiana na jeshi la Somalia kufanya operesheni kubwa  kaskazini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu na kuwatia mbaroni wapiganaji 62 wa kundi la Al-Shabab wakiwemo makamanda 22 wa kundi hilo. Wakati huo huo, mashirika ya kimataifa ya utoaji misaada yameendelea kusisitiza kwamba, kambi za wakimbizi nchini Somalia zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na kuongezeka idadi ya wakimbizi pamoja na vitisho vya kundi la Al-Shabab dhidi ya mashirika ya kimataifa yanayotoa misaada ya kibinadamu.

No comments:

Post a Comment