skip to main |
skip to sidebar
Wanajeshi wa Uingereza wapelekwa nchini Jordan
Duru za Magharibi zimetangaza kuwa wanajeshi wa Uingereza
wamepelekwa nchini Jordan ili kuendesha harakati dhidi ya Syria. Maafisa
wa duru za kuaminika jana walitangaza kuwa mamia ya wanajeshi na
washauri wa kijeshi wa Uingereza wametumwa huko Jordan ili kuendesha
harakati dhidi ya Syria na kuidhibiti nchi hiyo. Kabla ya hapo Leon
Panetta Waziri wa Ulinzi wa Marekani alitangaza kuwa wanajeshi maalumu
kutoka jeshi la
nchi hiyo wametumwa nchini Jordan ili kudhibiti hali ya
mambo katika mipaka ya Jordan na Syria. Wanajeshi wa Uingereza na
Marekani wametumwa Jordan ili kuimarisha nafasi yao katika machafuko
yanayoendelea huko Syria. Hii ni katika hali ambayo Jordan kila mwaka
hupokea msaada wa kijeshi kutoka Marekani wa thamani ya dola milioni 500
huku idara za kijasusi za nchi hiyo zikishirikiana na mashirika ya
Marekani.
No comments:
Post a Comment