Mamia ya Wakenya waliokuwa na hasira wamewashambulia Wasomali katika
mtaa wa Eastleigh, mjini Nairobi Kenya, ikiwa ni masaa machache tu
baada ya kutokea mlipuko kwenye shule ya Jumapili ya watoto wa Kikristo,
mlipuko ambao uliua mtoto mmoja na kujeruhi wengine kadhaa. Polisi
ililazimika kufanya kazi ya ziada kulitawanya kundi la vijana waliokuwa
na hasira ambalo lilikuwa likiwalenga Wasomali. Nyumba kadhaa za
Wasomali zimeshambuliwa kwa mawe katika shambulio hilo. Wakenya hao
wanawatuhumu Wasomali kuwa ndio waliohusika katika shambulio la bomu
hapo jana katika kanisa moja jijini Nairobi. Wasomali hao walilazimika
kukimbilia katika maduka au nyumba zao kuwakwepa vijana hao waliokuwa na
hasira. Wakati huo huo, maafisa wawili wa polisi ya Kenya wameuawa
katika mji wa Garissa eneo ambalo liko katika mpaka wa pamoja wa Kenya
na Somalia. Mlipuko wa jana na mauaji dhidi ya maafisa wawili wa polisi
yametajwa kuwa radiamali ya wanamgambo wa Ash Shabab wa Somalia baada ya
jeshi la Kenya kuudhibiti mji wa Kismayu ambayo ni ngome ya wanamgambo
hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment