skip to main |
skip to sidebar
Jeshi la Nigeria lakanusha tuhuma za kuua raia
Jeshi la Nigeria limekanusha kuwa askari wake juzi waliwaua watu 35
huko katika mji wa Maiduguri kaskazini mwa nchi hiyo. Watu walioshuhudia
wameeleza kuwa askari jeshi wa Nigeria walifyatua risasi baada ya bomu
kuripuka kwenye msafara wa jeshi na baadae askari jeshi hao wakaanza
kuwapiga raia kabla ya kuendelea na ufyatuaji risasi. Wauguzi katika
hospitali ya Umaru Shehu wamesema kuwa watu 30 waliouliwa na wanajeshi
walikuwa wamevaa nguo za kiraia huku wengine watano wakiwa na sare za
kijeshi. Luteni Kanali Sagir Musa ambaye ni msemaji wa kikosi cha pamoja
cha oparesheni huko katika jimbo la Borno amesema kuwa hakuna tukio
lolote linalohusisha kuuliwa raia hao 30 na kwamba kikosi hicho
hakikutekeleza uchomaji wowote wa mali za raia kwa makusudi wala
kuwatesa raia hao. Wanajeshi wa Nigeria wamekuwa wakituhumiwa mara kwa
mara kuwa wanaua raia na kuchoma nyumba au maduka yao kufuatia miripuko
ya mabomu inayowalenga wanajeshi hao
No comments:
Post a Comment