Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, October 11, 2012

Ndege za Israel zashambulia Ukanda wa Gaza



Ndege za Israel zashambulia Ukanda wa Gaza
Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel usiku wa kuamkia leo zimeshambulia maeneo kadhaa katika mji wa Bait Lahiya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza lakini bado hakujatangazwa idadi ya wahanga wa mashambulizi hayo.
Taarifa zinasema kuwa ndege za kijeshi za Israel zimerusha makombora kadhaa kaskazini mwa Gaza na kuzusha woga mkubwa kwa  wakazi wa eneo hilo.
Wakati huo huo vifaru na mabuldoza ya Israel yameingia katika eneo la mashariki la mji wa Rafah ikiwa ni katika kuendelea mashambulizi ya jeshi la utawala huo haramu yaliyoanza siku kadhaa zilizopita dhidi ya Gaza. Jeshi la Israel limethibitisha kuanza kwa mashambulizi hayo na kudai kwamba yanafanyika ili kujibu mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na Wapalestina dhidi ya utawala huo wa Kizayuni.

No comments:

Post a Comment