Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International limevikosoa
vikosi vya usalama vya Sudan Kusini kwa ukandamizaji dhidi ya raia wa
nchi hiyo. Mtandao wa habari wa Sudan Safari umechapisha ripoti
iliyotolewa na shirika hilo kuhusiana na mauaji na ukandamizaji wa
wanawake wa Sudan Kusini unaofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo.
Shirika hilo pia limetaka kuchukuliwa hatua za haraka kwa ajili ya
kukomesha aina hiyo ya uvunjwaji sheria. Kwa upande mwingine ripoti hiyo
imewanukuu wakazi wa mkoa wa Jonquil wa mashariki mwa nchi hiyo ambao
ndio wahanga zaidi wa vitendo hivyo na kusisitiza kuwa, wakazi hao
wanakabiliwa na hali mbaya ya mateso, kunyang'anywa mali na kuharibiwa mazao yao ya kilimo. Aidha kitengo cha masuala ya Kiafrika katika shirika hilo kimevituhumu vikosi vya usalama vya Sudan Kusini kwa kutotekeleza majukumu yao katika kukomesha vitendo hivyo. Kimesema kuna mashtaka chungu nzima na ya kutisha yanayovihusisha vikosi hivyo na uhalifu huo lakini kwamba serikali ya Juba imekataa kuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya wahalifu huku ikivitaja vitendo hivyo kuwa vidogo tu .

No comments:
Post a Comment