Maelfu ya Waislamu wameandamana nje ya makao makuu ya shirika la
Google mjini London Uingereza kulalamikia hatua ya U-tube ya kukataa
kuondoa filamu inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (s.a.w). Maandamano
hayo ya Waislamu elfu kumi ambayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Muslim
Action Forum yamefanyika ili kuilazimisha google kuondoa filamu hiyo
chafu katika ukurasa wa u-tube. Masoud Alam muandaaji wa maandamano hayo
ya London ameeeleza kuwa maandamano yao yajayo yatakuwa katika ofisi za
google na u-tube duniani kote. Amesema wanaandamana ili kuipiga
marufuku filamu hiyo dhidi ya matukufu ya Kiislamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment