Kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa
Al-Qaeda Ayman Al-Zawahiri amewashambulia vikali Marais Barack Obama wa
Marekani na Mohammad Mursi wa Misri akiwaita waongo na wasaliti wakubwa.
Kwenye kanda mpya ya video, kiongozi huyo wa Al-Qaeda amemtaka Rais
Obama kukiri kwamba Washington imeshindwa katika vita vya Iraq na
Afghanistan badala ya kuwahadaa Wamarekani kwamba nchi hiyo imefanikiwa
katika maeneo hayo. Amesema Marekani ililazimika kuondoka Iraq kwa
madhila na pia haina budi kuondoka Afghanistan kichwa chini. Akimhutubu
Rais wa Misri, al-Zawahiri ambaye ni mzaliwa wa Misri amesema Dkt. Mursi
ni msaliti ambaye baada ya kuingia madarakani alitupilia mbali takwa la
wanamapinduzi la kuundwa dola la Kiislamu. Ametoa wito kwa Wamisri
kuendelea na harakati za mapinduzi ili kuwang’oa vibaraka wa Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment