Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, October 26, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MSIKITI MPYA WA JIHAD WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Msikiti mpya wa Jihad, baada ya kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa Sikukuu ya Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya Kiislam katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi na waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka eneo hilo.

No comments:

Post a Comment