Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 15, 2012

Wapalestina wauawa na mashambulio ya Israel

Wapalestina wauawa na mashambulio ya Israel Wapalestina watano wameuawa shahidi katika wimbi jipya la jinai za jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza. Duru za kiusalama zinaripoti kutoka Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwamba, ndege za kijeshi za Israel zimefanya mashambulio katikati mwa Ukanda wa Gaza na kuwauwa shahidi Wapalestina watano huku makumi ya wengine wakijeruhiwa katika
mashambulio hayo. Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na makundi mbalimbali ya muqawama huko Palestina yamelaani vikali jinai hizo za Israel. Makundi ya muqawama huko Palestina yamebainisha kwamba, damu za mashahidi hazitapotea bure. Viongozi wa Palestina wanaamini kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha mashambulio yake huko Gaza katika siku za hivi karibuni ili kuzipotosha fikra za waliowengi ulimwenguni kuhusiana na matatizo makubwa ya ndani unayokabiliwa nayo.

No comments:

Post a Comment