
Zuma amejitokeza mbele ya vyombo vya habari na kusema matamshi ya makamu wake hayaakisi ukweli wa mambo kwani uchumi unasonga mbele na unakua kila siku. Hii ni katika hali ambayo viongozi hao wanatarajiwa kuchuana kwenye uchaguzi wa chama baadaye mwaka huu. Montlanthe amesema chama cha ANC kinahitaji mabadiliko kwani uongozi wa sasa umepoteza dira na kwa kiwango kikubwa umeitumbukiza nchi pabaya. Rais Zuma amekasirishwa na matamshi hayo na kusisitiza kuwa huo si msimamo rasmi wa serikali.
No comments:
Post a Comment