Watu wanne wameripotiwa kuuawa nchini Ethiopia akiwemo polisi
mmoja baada ya Waislamu waliokuwa wakiandamana kuvamia korokoro moja
wanakoshikiliwa Waislamu wenzao ambao wanatuhumiwa kuzusha ghasia.
Mauaji hayo ya Waislamu nchini Ethiopia yametokea baada ya kufanyika uchaguzi wa jumuiya ya Waislamu katika mji wa Gerba
katika mkoa wa Amhara.
Msemaji wa serikali ya Ethiopia Shimeles Kemal amesema kuwa watu watatu kati ya waandamanaji na polisi mmoja wameuawa katika ghasia zilizotokea baada ya waandamanaji hao kuvamia korokoro ya polisi wanakoshikiliwa Waislamu kadhaa kwa kosa ya kufanya maandamano kinyume cha sheria.
Mwezi Mei mwaka huu pia Waislamu wengine wanne waliuawa katika tukio kama hilo kwenye mji wa Oromia.
Waislamu wa Ethiopia wamekuwa wakifanya maandamano ya mara kwa mara wakipinga mwenendo wa serikali ya Addis Ababa wa kuingilia masuala ya yao ya kidini. Katiba ya Ethiopia inaizuia serikali kuingilia masuala ya kidini na kutangaza kuwa nchi hiyo inatawaliwa na mfumo wa kisekulari.

No comments:
Post a Comment