Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 15, 2012

Njama na vitimbi vyote vya maadui vitashindwa



'Njama na vitimbi vyote vya maadui vitashindwa' Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba, taifa la Iran linakabiliwa na vizingiti vingi, lakini litafanikiwa kuvuka vizuizi hivyo kwa kutumia uwezo wake, nguvu na hima kubwa. Ayatullahil Udhma Sayyid Ali khamenei amesema hayo leo katika siku yake ya nne ya kuutembelea mkoa wa Khorasan Kaskazini na kusisitiza kwamba, njama na vitimbi vyote vya maadui dhidi ya taifa hili vitashindwa.
Kiongozi Muadhamu amesema, maendeleo ya kimaada uliyoyapata ulimwengu wa Magharibi ikiwemo Marekani ni ya kidhahiri na yasiyo ya uhakika na kwamba, maendeleo na ustawi huu wa kidhahiri ambao una pengo la kimatabaka, chimbuko lake ni kuendeshwa nchi kwa mantiki ya kibepari na demokrasia ya kiliberali ya Magharibi. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, taifa la Iran hii leo liko katika vita vikubwa vya makabiliano baina ya irada na kwamba, licha ya kuweko vizingiti vingi, katu taifa hili halihisi udhaifu, bali litaweza kufikia malengo yake. Ayatullahil Udhma Khamenei ameashiria mikakati na njama kubwa za maadui za kulizuia taifa la Iran lisiendelee kujipatia maendeleo na kusisitiza kwamba, kama ambavyo njama za maadui zimekuwa zikigonga ukuta tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika kipindi hiki pia, njama, vitimbi na hila za maadui zitashindwa na wala hazitofikia popote.

No comments:

Post a Comment