Mh Ismail Jussa amewapongeza wanachi kwa kujitokeza kwao kwa wingi sana katika kongamano lilofanyika leo Bwawani. Pia ameipongeza kamati ya maridhiano kwa kitendo cha kuwakatisha tamaa wale wote wasioitakia mema Zanzibar.
Pia amemuomba MwenyeziMungu kumpa umri mrefu Mzee wetu Hassan Nassor
Moyo mpaka siku Zanzibar itakapokuwa huru na kwenda kupachika bendera
yake Umoja wa Mataifa na kuweza kutambulika kuwa ni nchi huru.
Amesema kuwa yeye binafsi hatachukua maamuzi yoyote yatakayokwenda
kinyume na chama chake hapa amekusudia kuwavunja moyo wale wasiojua kwa
nini amejiuzulu unaibu Katibu Mkuu jana ila lengo lake nikupata wasaa
nzuri wa kuongeza nguvu katika wimbi la kuitetea Zanzibar ndani ya
Baraza la Wawakilishi
Amesema ikiwa kuna makundi ya watu wenye nia ya kuvuvuruga maridhiano
yaliopo basi watavurugikwa wao kwa uwezo wa MwenyeziMungu alisistiza
kuwa kwa sasa tunataka Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na
kimataifa na sio Muungano huu wenye kuleta faida kwa upande mmoja tu
Amesema tunapodai nchi yetu hatutangazi vita na Tanganyika wala
isipokuwa ni kutaka kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ikifuatiwa na
Muungano wa Mkataba tu ndio jambo pekee kwa sasa wanalolitaka
Wazanzibari.
No comments:
Post a Comment