Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, October 21, 2012

‘Pesa haziwezi kufidia ukatili wa Uingereza Kenya’



‘Pesa haziwezi kufidia ukatili wa Uingereza Kenya’
Mwanaharakati mmoja wa Mau Mau amesema hakuna ‘kiasi chochote cha fedha’ kinachoweza kufidia ukatili uliotekelezwa na mkoloni Muingereza dhidi ya watu wa Kenya wakati wa kupigania uhuru wa nchi hiyo.
Katika mahojiano na Press TV Dr. Gitu wa Kahengeri, msemaji wa Jumuiya ya Maveterani wa Mau Mau waliopigania uhuru wa Kenya amesema; katika kesi ya Mau Mau dhidi ya serikali ya Uingereza suala la pesa si muhimu bali suala muhimu ni Uingereza ikiri kutenda jinai na iombe msamaha.  Aidha katika mahojiano na Press TV Esther Stanford-Xosei , mwanaharakati wa kutetea Waafrika walipewe fidia na madola ya kikoloni Ulaya amesema  wanaharakati wa Mau Mau hawatapata uadilifu wanaotafuta katika mahakama za Uingereza.  Mau Mau wamewasilisha kesi katika mahakama kuu ya Uingereza wakitaka fidia kutokana na jinai zailizotekelezwa na wa utawala wa kikoloni ya Uingereza nchini Kenya kati ya mwaka 1952 na 1961. Tume ya Haki za Binaadamu Kenya imesema Wakenya 90,000 waliteswa au kuuawa katika kipindi hicho, na watu 160,000 waliwekwa kizuizini katika mazingira ya kuogofya.

No comments:

Post a Comment