
vijiji kadhaa vya Waislamu wa kaskazini magharibi mwa Myanmar vimeteketezwa kwa moto na Mabudha wanaosaidiwa na jeshi la polisi, na wakazi wa vijiji hivyo wamelazimika kuwa wakimbizi. Mabudha hao wenye misimamo mikali pia wamechoma moto misikiti kadhaa. Umoja wa Mataifa umesema kuwa ukatili wanaofanyiwa Waislamu wa Myanmar ndiyo mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa duniani katika siku za hivi karibuni. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema kuwa jeshi la Myanmar limetenda jinai nyingi dhidi ya Waislamu wa Rohingya walio wachache. Ripoti hiyo imefafanua kuwa miongoni mwa jinai hizo ni kubakwa wanawake wa jamii hiyo ya Waislamu kaskazini mwa Myanmar.
No comments:
Post a Comment