Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, October 30, 2012

Ghasia zaendelea Kisumu kwa siku ya pili



Ghasia zaendelea Kisumu kwa siku ya pili
Ghasia na machafuko yameendelea kwa siku ya pili mfululizo katika mji wa maghribi mwa Kenya wa Kisumu baada ya mauaji ya jana ya mwanasiasa wa chama cha ODM.
Polisi ya Kenya imetumia gesi ya kutoa machozi kujaribu kuwatawanya mamia ya vijana waliokuwa wakiandamana kupinga mauaji ya Shem Onyango Kwega, aliyetarajiwa kugombea kiti cha ubunge kwa tiketi ya chama cha Waziri Mkuu Raila Odinga ODM katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwakani.
Kwega ambaye alikuwa mwenyekiti wa tawi la chama cha ODM huko Kisumu aliuawa jana kwa kigwa risasi akiwa pamoja na mkewe wake. Mke wa wanasiasa huyo naye amejeruhiwa vibaya na yuko mahututi hispitalini.
Chama cha ODM kimelaani mauaji hayo na kimetoa wito wa kufanyika uchunguzi.
Watu wengine wanne waliuawa jana katika ghasia zilizohusisha waandamanaji na polisi ya Kenya na wengine kadhaa walijeruhiwa.

No comments:

Post a Comment