Taarifa kutoka visiwani Zanzibar nchini Tanzania zinasema kuwa, hali
ya usalama visiwani humo bado sio shwari kufuatia kutoweka katika hali
ya kutatanisha kiongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Uamasho Sheikh Farid
Hadi Ahmed. Hali ya taharuki na machafuko ilianza kushuhudiwa katika
maeneo ya mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Ungauja hapo jana baada
kuenea taarifa za kukamtawa na kutekwa nyara na watu wasiojulikana
Sheikh Farid ambaye pia ni msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Zanzibar. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa askari mmoja wa kikosi cha
kutuliza ghasia cha FFU ameuawa kwa kupigwa mapanga na kukatwa kichwa na
watu wasiojulikana huku kukishuhudiwa pia vitendo kadhaa vya uhalifu
ikiwa ni pamoja na kuchomwa moto nyumba za wageni, maskani ya CCM ya
Kisonge mjini Unguja, maeneo ya biashara na hata mali za wananchi.
Katika hali ambayo vyombo vya usalama vinayahusisha matukio hayo na
wafuasi wa Uamsho, Katibu wa jumuiya hiyo Sheikh Abdullah Said
amekanusha tuhuma hizo na kusema kwamba wafuasi wa taasisi hiyo ya
Kiislamu hawahusiki na vitendo hivyo. Taarifa zaidi zinasema kuwa,
machafuko hayo yanashuhudiwa zaidi katika maeneo ya Darajani,
Michenzani, Muembeladu, Magomeni na Amani. Wakati huo huo Kamishna wa
Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa amesema kuwa, Sheikh Farid amepotea
katika hali ya kutatanisha, na kwamba hadi sasa juhudi za kumtafuta bado
zinaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment