Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 8, 2012

Tanzania yaitaka Malawi irudi katika mazungumzo


Tanzania yaitaka Malawi irudi katika mazungumzoTanzania imeiomba Malawi irudi katika meza ya mazungumzo kuhusu mzozo wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya nchi hizo mbili.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tanzania Bernard Membe alipozungumza na waandishi habari jijini Dar-es-Salaam siku ya Jumamosi. Membe ameiomba serikali ya Malawi kutuma wawakilishi katika kikao walichokubaliana kufanyika kwa siku nne jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kinakusudia kupendekeza mpatanishi ambaye atakubalika na pande zote baada ya kubainika kuwa Tanzania na Malawi zenyewe hazitaweza kusuluhisha mzozo huo. Malawi imesema haitashiriki katika hicho kwa sababu Tanzania imetuma boti yake ya kijeshi katika Ziwa Nyasa. Malawi pia inataka kupatiwa maelezo kuhusu toleo jipya la Ramani ya Tanzania ambayo inaonesha mpaka baina ya nchi hizo mbili umepita katikati ya Ziwa Nyasa.
Membe amesema Tanzania itapendekeza mpatanishi hataka kama Malawi haitarudi katika mezi ya mazungumzo. Ziwa Malawi au Ziwa Nyasa ndio ziwa la tatu kwa ukubwa barani Afrika na inaaminika kuwa lina utajiri mkubwa wa mafuta na gesi.

No comments:

Post a Comment